Settings
Light Theme
Dark Theme
Podcast Cover

Tanzania Gnosis's podcast

  • Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 3)

    17 MAR 2024 · Maarifa ya ndani ni kazi ya kiungu ndani ya mwanadamu. Maarifa haya hayahusiani na akili (intellect). Maarifa ama ujuzi hufahamika kwa Kiebrania kama "Daath". Maarifa yanaweza kusababisha uzima ama mauti kwa mtu, itategemeana na kazi za matendo yake. Katika masomo haya, tunapata kuona ya kwamba Muumba huumba kwa kupitia Maarifa na kwamba Muumba ndani yetu ni yule hufahamika kama Ruach Elohim (ama Ruach El Ha'yam). Idadi ya neno "Ruach Elohim" katika hesabu za herufi hizo ni jumla 300. Hii 300 ni thamani ya herufi ya Kiebrania Shin ש amapo herufi hii huwa na maana ya moto. Huu ndiyo moto ambao hufanya kazi ndani ya kila mtu. Hii ni sababu pekee ya kwamba tunapotizama neno mwanaume kwa Kiebrania ni neno "ish איש", kadhalika neno mwanamke kwa Kiebrania ni neno "ishah אשה". Tunaposoma kitabu cha Mwanzo (Bereshit) tunajifunza kwamba wawili hawa hawaitwi Adam wala Eva isipokuwa ni baada ya kufukuzwa ndani ya bustani. Vile vile tunapotizama neno mwanaume yaani ish איש tunagundua kwamba tukiondoa herufi Yod י kinachosalia husomeka "esh אש" ambayo ina maana ya "moto", kadhalika neno mwanamke yaani ishah אשה tukiondoa herufi Hei ה tunasalia na neno "esh אש" ambalo lina maana ya "moto". Yod י ni herufi kiume enye maana ya uume. Kadhalika Hei ni herufi kike enye maana ya uke. Hizi ndizo tofauti kuu za msingi zinazotofautisha mwanaume na mwanamke yaani kwa maana ya jinsia. Moto huu ni kazi ya Ruach Elohim ambaye ni baba aliye sirini kwa kila mtu. Moto huu unapotumiwa kwa usahihi yaani kwa mema (tov טוב) huwa ni sababu ya wokovu kwa nafsi lakini unapotumiwa kimakosa yaani kwa mabaya (ra רע) huwa ni sababu ya kuangamia kwa nafsi. Karibu kujifunza maarifa haya kwa kina. Ikiwa una maoni ama maswali ama ushauri, tuandikie kwa baruapepe ya: tanzaniagnosishelpers@gmail.com Maarifa nuwa na matokeo ya moto
    1h 26m 50s
  • Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 2)

    25 FEB 2024 · Nyoka hufahamika kama shetani na inaandikwa hivyo. Lakini wanadamu wa tabia za mwili hawafahamu upande wa pili wa kile kinachofahamika kama nyoka! Neno la Kiebrania Tov טוב lina maana na "mema" lakini ndani ya hayo mema tunaona kuna herufi ya Kiebrania Tet ט enye maana ya "nyoka" kadhalika herufi hiyo hiyo ni namba 9. Katika maarifa ya Kabbalah namba 9 ni ukamilifu wa neno Adam אדם na ndiyo maana kwa kuzingatia pia ya kwamba Kabbalah ni maarifa ya namba, katika numerologia tunaona kwamba ndani ya neno Adam kuna herufi Aleph א, Daleth ד na Mem ם (final), ambapo: • Aleph א ni namba 1 • Daleth ד ni namba 4 • Mem ם ni namba 40 Numerologia huzingatia namba 0 hadi 9 maana namba yoyote juu ya 9 ni marudio kati ya 0 hadi 9 yenyewe. Hivyo tunajumlisha kwa namna hii: 1+4+4+0=9 Hii tunaona ndiyo sababu mwanadamu hukaa miezi 9 tumboni mwa mamaye. Turejee ya kwamba namba 9 ni ile herufi Tet ambayo ina maana ya nyoka. Vile vile nyoka hakuondolewa ndani ya bustani ya Eden mara baada ya anguko kwa Adam na Eva ila tunaona wawili hawa ndiyo waliondolewa. Kitendo cha kuondolewa Eden ni kile tunachokiita mwanadamu kuzaliwa katika mwili wa damu na nyama yaani huu mwili wa uharibifu. Na ndiyo maana kwa asili kila mwanadamu ni mwana wa Adam kwa maana ya 9 yaani herufi Tet ט katika namna ya anguko. Hii ni sababu wengi hawaelewi ni kwanini rabbi Yesu alisema: Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Mathayo 23:33 Wana wa majoka ni wana wa herufu Tet ט katika anguko yaani nje ya bustani ya Eden hivyo tunalithibitidha hilo katika maarifa kwa kile kinachotokea yaani nafsi kuja katika mwili katika ukamilifu wa 9 yaani kwa kupitia miezi 9. Tukiwa katika mwili rabbi Yesu akasema: ..basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. Mathayo 10:16b Kuwa na busara kama nyoka huu ni upande mwingine tofauti wa kile kinachofahamika kama nyoka. Huyu ni nyoka wa Musa. Huyu ni yule nyoka wa Brasi (na siyo shaba kama inafvitafsiriwa) ambaye Musa alimwinua kwa ajili ya uponyaji wa wana wa Israeli. Mambo haya hunenwa kwa maarifa na si kimtizamo kusoma literally kama simulizi za kawaida. Brasi (brass) ni muunganiko wa Zinki (zinc) na Shaba (copper) ambapo Zinki inawakilisha Adam na Shaba inawakilisha Eva. Matokeo ya muunganiko huko ndiyo kuinuliwa kwa nyoka ambapo katika neno Tov טוב lenya maana ya "mema", herufi ya mwisho ni Beth ב yenye maana ya hekalu/hema ambayo ina maanisha miili yetu na ndiyo maana miili yetu ni bustani ambapo herufi Vav ו ni mti (wa uzima) ambayo nyoka wa Brasi (Zinki+Shaba) yaani herufi Tet ט hutundikwa kwa ajili ya ya uzima. Nyoka anapomshinda mwanadamu kwa jaribu huitwa shetani wakati nyoka anayeshindwa, kwa washindi huwa ni busara. Ndiyo maana ya kile asemacho rabi Yesu "..iweni na busara kama nyoka". Kadhalika hiki ndicho kile rabbi Yesu akimwambia Nikodemo: Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; Yohana 3:14 Mambo haya hupaswa kufanyika ndani yetu. Kwa mengine zaidi, karibu tujifunze pamoja. Unaweza wasiliana nasi kwa barua pepe: tanzaniagnosishelpers@gmail.com
    58m 5s
  • Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 1)

    18 FEB 2024 · Neno "mema na mabaya" kwa Kiebania ni טוב ו רע (tov ve ra). Tov טוב ikiwa na herufi tatu yaani Tet ט, Vav ו na Beth ב. Kadhalika Ra רע ikiwa na herufi Resh ר na Ayin ע. Tatika Tov טוב tunapata kufahamu maana iliopo katika kila herufi zilizofanya neno hilo yaani: • Tet ט ikiwa na maana ya nyoka (serpent) na vile vile ikiwa na thamani ya namba 9. • Vav ו ikiwa na maana ya uti wa mgongo ama mti/fimbo na vile vile ikiwa na thamani ya namba 6. • Beth ב ikiwa na maana ya nyumba/hema/hekalu na vile vile ikiwa na thamani ya namba 2. Katika neno "Mema" yaani Tov kwa habari ya herufi ya kwanza yaani Tet ט tunapata kujifunza juu ya nyoka mjaribu ambaye siku zote yumo ndani ya bustani na wala baana ya kosa lililotokea hakufukuzwa ndani ya bustani isipokuwa ni Adam na Eva. Katika undani wetu kwa kuzingatia maarifa ya ndani yetu sisi ni bustani sisi ni nyumba yaani herufi ya mwisho Beth ב (ya kwenye neno Tov טוב). Kadhalika tunajifunza juu ya herufi ya pili Vav ו ambayo ndiyo uti wa mgongo na vile vile enye thamani ya namba 6 sawa sawa na siku za uumbaji katika kitabu cha Mwanzo uumbaji huu unaakisi uumbaji wa nafsi ya mwanadamu katika sehemu muhimu sita ndani yake. Herufi Vav pia bila kusahau ni kiunganishi "na" ama "and" kwa Kiingereza. Vile vile herufi Vav ו inatukumbusha kwamba Mungu anapofanya uumbaji, kufanya kwa kupitia herufi Vav ו kwa kuzingatia uti wa mgongo. Hii ndiyo sababu pekee ya kwamba tunaposoma kitabu cha Mwanzo sura ya 1 mara nyingi inaandikwa "and God said" hii "and" inayotangu lia kabla ya God ni herufi Vav ו. Kwa bahati isiyo nzuri tunaposoma Biblia ya Kiswahili (SUV) hatukutani na utangulizi wa kiunganishi "na" kama ilivyo katika Biblia ya tafsiri ya Kiingereza (KJV). Ndiyo maana kuna umuhimu kwa wasomi wa Biblia kufahamu uandishi wake katika lugha yake asili na siyo tu kutizamia haya katika tafsiri na kudhani kwamba tumeelewa maatifa yaliyoandikwa ndani yake. Mtume Paulo ni Kabbalist na aliandika mambo haya kwa wenye uwezo wa kusikia maarifa ya Kabbalah akisema kkatika moja ya nyaraka zake: "Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu." 1 Wakorintho 3:9 — Shamba ni kwa maana ya bustani [Eden] na vilevile jengo ni kwa maana ya herufi Beth ב ambamo ndani yake ndipo Muumba hufanya makao yake. Katika maatifa ya ndani ni rahisi kwetu kuelewa ya kwamba Bwana Mungu alipomuumba mtu inaandikwa: Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. Mwanzo 2:15 — Ni kitendo cha maarifa kufahamu ya kwamba nafsi ya mwanadamu ndiyo inayowekwa ndani ya mwili ambao ndilo shamba la Mungu ili mwanadamu alime na kulitunza. Jambo hili ni kati ambayo hutendwa kwa ushirikiano kati ya Mungu na mwanadamu mwenye maarifa (Daath) na ndiyo maana ya kile tulichokisema kwamba Mungu huumba kwa kupitia uti wa mgongo yaani herufi Vav ו ambayo pia ni kiunganishi "na" na ndiyo inaandikwa inaandikwa "na Mungu akasema..", "..na Mungu akaona..", "na Mungu akafanya" n.k Katika neno "Mabaya" yaani Ra tunapata kujifunza juu ya herufi mbili. Herufi Resh ר ambayo ina maana ya Kichwa (ambapo ndani yetu Adam anawakilishwa na ubongo). Vile vile herufi Ayin ע ambayo inamaana ya jicho lakini vile vile ni ile namna ya upeo wa utambuzi wa mambo kwa kina. Tulijifunza katika somo lililopita ya kwamba Ayin ע ni herufi ya Kiebrania yenye maana ya jicho lakini jicho hili linaweza kuwa ni jicho la nuru au tunasema la Kiungu ama la giza ambalo waaguzi hulitumia. Mwanadamu anapojaribiwa na nyoka (Herufi Tet ט) na kuanguka, nyoka hufumbua jicho lake na kumpa kuona lakini Mungu hayupo katika uwezo huo wa kuona na ndiyo maana kinachoendelea ni Ra yaani uovu ama mabaya ndani ya kichwa (herufi Resh ר) cha muhusika. Tunapaswa tuweze kuona katika jicho la kiroho lakini katika namna ya maarifa (Daath) ya Kiungu. Tunakukaribisha kujifunza maarifa haya ya ndani.
    1h 24m 14s
  • Mti wa Ujuzi - 2. Maarifa (Ujuzi), Adam na Eva ndani yetu

    10 FEB 2024 · Tunapozungumzia Adam tunapata tafsiri ya mwanaume, kadhalika Eva, mwanamke. Katika maarifa ya ndani tunapata kufahamu ya kwamba Adam na Eva ni uhusika ambao unakamilisha uhalisia wetu sisi wenyewe. Adam na Eva ni mikondo miwili ya nishati inayofanya kazi kwa pamoja na tena kwa ushirikiano. Mikondo hii hufahamika kwa lugha ya kale (Sanskrit) huko India kama PINGALA na IDA, vile vile kwa Kiebrania katika maarifa ya Kabbalah hufahamika kama OD na OB. Kwa kuzingatia hayo, vile vile ni muhimu sana kufahamu ya kwamba Adam na Eva ndani ya miili yetu huwakilishwa na UBONGO na VIA VYA UZAZI. Adam kama ubongo iwe no ubongo wa mwanaume ama wa mwanamke, na Eva kama via vya uzazi, iwe ni via vya uzazi vya kike ama vya kiume, vyote husimama nafasi ya Eva. Eva (via vya uzazi) anajaribiwa na kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya lakini pia ili ampatie Adam (ubongo) ili naye ale inampasa kunyosha mkono (kwa kupitia uti wa mgongo ambao una pingili 33). Hizi pingili 33 katika maarifa ya kinumerolojia ndani ya Kabbalah ni sawa na 3+3 ambayo ni 6. Uti wa mgongo katika maarifa ya Kabbalah huwakilishwa na herufi Vav (ו) ya Kiebrania ambayo vilevile ni herufi ya 6 kimpangilio na ina thamani ya namba 6. Amri ya 6 inasema "usizini" lakini pia uumbaji unafanywa kwa siku 6 bila kusahau ya kwamba mwanadamu anaumbwa siku ya 6. Karibu ujifunze pamoja nasi katika elimu ya ndani ya Gnosis.
    50m 12s
  • Mti wa Ujuzi - 1. Maarifa (Ujuzi), Mlango

    4 FEB 2024 · Mti wa ujuzi ni elimu ya kiroho inayohusiana na nafsi ya mwanadamu. Mwili wa mwanadamu ni chombo kinachobeba nafsi na roho hivyo hatuwi na miili kana kwamba haina cha kufanya ambacho kinahusiana na ukombozi wa nafsi zetu. Kumekuwa mkanganyiko wa mafundisho juu ya elimu nzima inayohusiana na bustani ya Eden pamoja na mwanaume na mwanamke yaani Adam na Eva ndani ya bustani. Vizazi vilivyotangulia vilikuwa na uhodari wa kuficha maarifa kwa maana si kitu ambacho kila akipataye hukitumia kwa mtizamo chanya. Ni watu wachache sana waliochaguliwa ambao waliweza kupana nafasi ya kujifunza. Kwa kipindi kirefu sana kilichopita, maarifa haya yalifundishwa kwa wachache lakini nyakati zimefika, maarifa kufundishwa kwa kizazi hiki cha sasa. Maarifa ama ujuzi ni neno "Da'ath דעת" kwa Kiebrabia. Neno hili "Da'ath דעת" ni muunganiko wa herufi za Kiebrania tatu: Daleth ד, Ayin na Tav ת. Pia, zingatia kwamba maneno ya lugha ya Kiebrania husomwa kuanzia upande wa kuume (kulia) kuelekea kushoto. Karibu sana darasani.
    37m 51s
  • Maarifa ya Asili (Utangulizi)

    4 FEB 2024 · Gnosis siyo dini kana kwamba watu wake ni wa kutafuta kukusanya watu na kuanzisha nyumba za ibada. Gnosis ni maatifa ya ndani ambayo huambatana na juhudi katika natendo hata kupata matokeo chanya. Wana-gnosis tunaheshimu dini zote maana tunapotizama mafundisho yake tunakuta ni kivuli ya majukumu ambayo kila mwana-gnosis hupaswa kupitia yaani njia yenyewe ya kuelekea nuruni. Njia ya Gnosis haijihusishi na kunyoshea watu vidole wala hatujikwezi ya kwamba sisi ni bora kuliko yeyote. Tunatambua jukumu la kubadilika sisi kwanza ili wengine nao wabadilike na siyo kupambana kuona mabovu ya wengine huku ya kwetu hatuyaoni. Kila mwana-gnosis huipita njia ya maarifa hatua kwa hatua, kupanda na kushuka hata kuufikia ukamilifu. Pamoja na kwamba mwana-gnosis atafikia kizio cha juu ya utimilifu, hakupo kujikweza kusema kwamba yeye ni bora kuliko fulani. Vilevile ni siri ya mtu kusema kizio alichofikia kwa maana kizio afikiacho mtu ni ya ndani yake na wala hakihusiani na mwili huu wa uharibifu. Ndiyo maana tunajifunza maarifa ya ndani ambayo hayahusiani kabisa na maarifa ya akili (intellectual mind). Utajifunza maarifa yatokanayo na utu wa ndani kwa faida za nafsi yako. Kwa maana ni muhimu sana kuyafahamu maarifa ya ndani yako na mengine yote huja kama mshahara wa ufahamu wako juu ya Muumba aliye ndani yako. Maarifa haya siyo yale yaliyozoeleka yaani ya mwili ama ya kiakili, la hasha. Pamoja na yoye, ni kwamba tunatumia mwili kama ni mlango wa kutupitisha kule tuendako kwa maana tupo kwenye miili kwa kusudi maalumu.
    1h 26m 27s

Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni -...

show more
Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni - ni maarifa, uzoefu, si ujuzi wa kiakili au dhana tu, imani, au nadharia. Neno hili ni sawa na neno la Kiebrania "Daath" na la Sanskrit "Jna."
show less
Contacts
Information

Looks like you don't have any active episode

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Current

Looks like you don't have any episodes in your queue

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Next Up

Episode Cover Episode Cover

It's so quiet here...

Time to discover new episodes!

Discover
Your Library
Search