Settings
Light Theme
Dark Theme

Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 1)

Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 1)
Feb 18, 2024 · 1h 24m 14s

Neno "mema na mabaya" kwa Kiebania ni טוב ו רע (tov ve ra). Tov טוב ikiwa na herufi tatu yaani Tet ט, Vav ו na Beth ב. Kadhalika Ra רע...

show more
Neno "mema na mabaya" kwa Kiebania ni טוב ו רע (tov ve ra). Tov טוב ikiwa na herufi tatu yaani Tet ט, Vav ו na Beth ב. Kadhalika Ra רע ikiwa na herufi Resh ר na Ayin ע.

Tatika Tov טוב tunapata kufahamu maana iliopo katika kila herufi zilizofanya neno hilo yaani:

• Tet ט ikiwa na maana ya nyoka (serpent) na vile vile ikiwa na thamani ya namba 9.

• Vav ו ikiwa na maana ya uti wa mgongo ama mti/fimbo na vile vile ikiwa na thamani ya namba 6.

• Beth ב ikiwa na maana ya nyumba/hema/hekalu na vile vile ikiwa na thamani ya namba 2.

Katika neno "Mema" yaani Tov kwa habari ya herufi ya kwanza yaani Tet ט tunapata kujifunza juu ya nyoka mjaribu ambaye siku zote yumo ndani ya bustani na wala baana ya kosa lililotokea hakufukuzwa ndani ya bustani isipokuwa ni Adam na Eva. Katika undani wetu kwa kuzingatia maarifa ya ndani yetu sisi ni bustani sisi ni nyumba yaani herufi ya mwisho Beth ב (ya kwenye neno Tov טוב). Kadhalika tunajifunza juu ya herufi ya pili Vav ו ambayo ndiyo uti wa mgongo na vile vile enye thamani ya namba 6 sawa sawa na siku za uumbaji katika kitabu cha Mwanzo uumbaji huu unaakisi uumbaji wa nafsi ya mwanadamu katika sehemu muhimu sita ndani yake. Herufi Vav pia bila kusahau ni kiunganishi "na" ama "and" kwa Kiingereza.

Vile vile herufi Vav ו inatukumbusha kwamba Mungu anapofanya uumbaji, kufanya kwa kupitia herufi Vav ו kwa kuzingatia uti wa mgongo. Hii ndiyo sababu pekee ya kwamba tunaposoma kitabu cha Mwanzo sura ya 1 mara nyingi inaandikwa "and God said" hii "and" inayotangu lia kabla ya God ni herufi Vav ו. Kwa bahati isiyo nzuri tunaposoma Biblia ya Kiswahili (SUV) hatukutani na utangulizi wa kiunganishi "na" kama ilivyo katika Biblia ya tafsiri ya Kiingereza (KJV). Ndiyo maana kuna umuhimu kwa wasomi wa Biblia kufahamu uandishi wake katika lugha yake asili na siyo tu kutizamia haya katika tafsiri na kudhani kwamba tumeelewa maatifa yaliyoandikwa ndani yake.

Mtume Paulo ni Kabbalist na aliandika mambo haya kwa wenye uwezo wa kusikia maarifa ya Kabbalah akisema kkatika moja ya nyaraka zake:

"Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu."
1 Wakorintho 3:9

— Shamba ni kwa maana ya bustani [Eden] na vilevile jengo ni kwa maana ya herufi Beth ב ambamo ndani yake ndipo Muumba hufanya makao yake.

Katika maatifa ya ndani ni rahisi kwetu kuelewa ya kwamba Bwana Mungu alipomuumba mtu inaandikwa:

Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 2:15

— Ni kitendo cha maarifa kufahamu ya kwamba nafsi ya mwanadamu ndiyo inayowekwa ndani ya mwili ambao ndilo shamba la Mungu ili mwanadamu alime na kulitunza. Jambo hili ni kati ambayo hutendwa kwa ushirikiano kati ya Mungu na mwanadamu mwenye maarifa (Daath) na ndiyo maana ya kile tulichokisema kwamba Mungu huumba kwa kupitia uti wa mgongo yaani herufi Vav ו ambayo pia ni kiunganishi "na" na ndiyo inaandikwa inaandikwa "na Mungu akasema..", "..na Mungu akaona..", "na Mungu akafanya" n.k

Katika neno "Mabaya" yaani Ra tunapata kujifunza juu ya herufi mbili. Herufi Resh ר ambayo ina maana ya Kichwa (ambapo ndani yetu Adam anawakilishwa na ubongo). Vile vile herufi Ayin ע ambayo inamaana ya jicho lakini vile vile ni ile namna ya upeo wa utambuzi wa mambo kwa kina. Tulijifunza katika somo lililopita ya kwamba Ayin ע ni herufi ya Kiebrania yenye maana ya jicho lakini jicho hili linaweza kuwa ni jicho la nuru au tunasema la Kiungu ama la giza ambalo waaguzi hulitumia.

Mwanadamu anapojaribiwa na nyoka (Herufi Tet ט) na kuanguka, nyoka hufumbua jicho lake na kumpa kuona lakini Mungu hayupo katika uwezo huo wa kuona na ndiyo maana kinachoendelea ni Ra yaani uovu ama mabaya ndani ya kichwa (herufi Resh ר) cha muhusika.

Tunapaswa tuweze kuona katika jicho la kiroho lakini katika namna ya maarifa (Daath) ya Kiungu.

Tunakukaribisha kujifunza maarifa haya ya ndani.
show less
Information
Author Tanzania Gnosis
Website -
Tags
-

Looks like you don't have any active episode

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Current

Looks like you don't have any episodes in your queue

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Next Up

Episode Cover Episode Cover

It's so quiet here...

Time to discover new episodes!

Discover
Your Library
Search