Settings
Light Theme
Dark Theme

Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 2)

Mti wa Ujuzi - 3. Maarifa (Ujuzi), Mema na Mabaya (Seh. 2)
Feb 25, 2024 · 58m 5s

Nyoka hufahamika kama shetani na inaandikwa hivyo. Lakini wanadamu wa tabia za mwili hawafahamu upande wa pili wa kile kinachofahamika kama nyoka! Neno la Kiebrania Tov טוב lina maana na...

show more
Nyoka hufahamika kama shetani na inaandikwa hivyo. Lakini wanadamu wa tabia za mwili hawafahamu upande wa pili wa kile kinachofahamika kama nyoka! Neno la Kiebrania Tov טוב lina maana na "mema" lakini ndani ya hayo mema tunaona kuna herufi ya Kiebrania Tet ט enye maana ya "nyoka" kadhalika herufi hiyo hiyo ni namba 9. Katika maarifa ya Kabbalah namba 9 ni ukamilifu wa neno Adam אדם na ndiyo maana kwa kuzingatia pia ya kwamba Kabbalah ni maarifa ya namba, katika numerologia tunaona kwamba ndani ya neno Adam kuna herufi Aleph א, Daleth ד na Mem ם (final), ambapo:

• Aleph א ni namba 1
• Daleth ד ni namba 4
• Mem ם ni namba 40

Numerologia huzingatia namba 0 hadi 9 maana namba yoyote juu ya 9 ni marudio kati ya 0 hadi 9 yenyewe. Hivyo tunajumlisha kwa namna hii:

1+4+4+0=9

Hii tunaona ndiyo sababu mwanadamu hukaa miezi 9 tumboni mwa mamaye. Turejee ya kwamba namba 9 ni ile herufi Tet ambayo ina maana ya nyoka. Vile vile nyoka hakuondolewa ndani ya bustani ya Eden mara baada ya anguko kwa Adam na Eva ila tunaona wawili hawa ndiyo waliondolewa.

Kitendo cha kuondolewa Eden ni kile tunachokiita mwanadamu kuzaliwa katika mwili wa damu na nyama yaani huu mwili wa uharibifu. Na ndiyo maana kwa asili kila mwanadamu ni mwana wa Adam kwa maana ya 9 yaani herufi Tet ט katika namna ya anguko. Hii ni sababu wengi hawaelewi ni kwanini rabbi Yesu alisema:

Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
Mathayo 23:33

Wana wa majoka ni wana wa herufu Tet ט katika anguko yaani nje ya bustani ya Eden hivyo tunalithibitidha hilo katika maarifa kwa kile kinachotokea yaani nafsi kuja katika mwili katika ukamilifu wa 9 yaani kwa kupitia miezi 9. Tukiwa katika mwili rabbi Yesu akasema:

..basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Mathayo 10:16b

Kuwa na busara kama nyoka huu ni upande mwingine tofauti wa kile kinachofahamika kama nyoka. Huyu ni nyoka wa Musa. Huyu ni yule nyoka wa Brasi (na siyo shaba kama inafvitafsiriwa) ambaye Musa alimwinua kwa ajili ya uponyaji wa wana wa Israeli. Mambo haya hunenwa kwa maarifa na si kimtizamo kusoma literally kama simulizi za kawaida.

Brasi (brass) ni muunganiko wa Zinki (zinc) na Shaba (copper) ambapo Zinki inawakilisha Adam na Shaba inawakilisha Eva. Matokeo ya muunganiko huko ndiyo kuinuliwa kwa nyoka ambapo katika neno Tov טוב lenya maana ya "mema", herufi ya mwisho ni Beth ב yenye maana ya hekalu/hema ambayo ina maanisha miili yetu na ndiyo maana miili yetu ni bustani ambapo herufi Vav ו ni mti (wa uzima) ambayo nyoka wa Brasi (Zinki+Shaba) yaani herufi Tet ט hutundikwa kwa ajili ya ya uzima.

Nyoka anapomshinda mwanadamu kwa jaribu huitwa shetani wakati nyoka anayeshindwa, kwa washindi huwa ni busara. Ndiyo maana ya kile asemacho rabi Yesu "..iweni na busara kama nyoka". Kadhalika hiki ndicho kile rabbi Yesu akimwambia Nikodemo:

Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
Yohana 3:14

Mambo haya hupaswa kufanyika ndani yetu.

Kwa mengine zaidi, karibu tujifunze pamoja.

Unaweza wasiliana nasi kwa barua pepe:
tanzaniagnosishelpers@gmail.com
show less
Information
Author Tanzania Gnosis
Website -
Tags
-

Looks like you don't have any active episode

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Current

Looks like you don't have any episodes in your queue

Browse Spreaker Catalogue to discover great new content

Next Up

Episode Cover Episode Cover

It's so quiet here...

Time to discover new episodes!

Discover
Your Library
Search